Mtoto ni wako

Wao husema eti mtoto hulelewa na jamii
Kwa hivyo kila kitendo kwa mtoto
Umemtendea mwana wako.
Mtoto alitembea kuingia kwenye klabu
Ukamwingiza
Mtoto ulimwuzia pombe na dawa za kulevya
Ulimwuzia mtoto wako.

Msichana ulimwona akitembea barabarani
Uliamua kumfanyia kile kitendo cha aibu
Binti huyo ni wako.
Mtoto alitumwa dukani
Ulimdanganya na peremende ili kumteka
Ulimteka mtoto wako.

Ulimdanganya mamake mzazi
Utamsomesha mwanawe
Lakini unafanya ajira ya watoto
Mtoto huyo ni wako.
Mzazi amnyima mtoto elimu
Wakuu wakitazama
Hata nyinyi mnaotazama mtoto ni wako.

Ni kweli hukuchangia kitendo cha kibayolojia
Lakini mtoto anabaki kuwa wako
Kwani ni wetu sote tumlinde mtoto wetu
Simamia mtoto wako
Mtoto wa jamii

Mtoto ni wako.