Viumbe Vyote Vya Mungu Wetu

Mlalahoi na mlalahai, mchokoropipa,meneja wa benki, daktari, kasisi na mkulima , mwalimu na mwanafunzi, mrefu na mfupi, waume na wake, kiziwi, kipofu na mlemavu. Kijana na Mzee.
Wote ni viumbe vya Maulana wetu.
Ama hujawahi kusikia wimbo huu…
Viumbe vyote vya Mungu wetu na mfalme wetu..
Viumbe vyote vya Mungu wetuetu na mfalme wetu…
Wote wanapendwa na Mola. Hakuna mmoja zaidi ya mwingine. Hakuna aliye juu ya mwingine.
Sote alitupenda. Ndiposa akafa msalabani.
Sote tu sawa mbele yake. Hakuna mkubwa kwake. Hakuna mdogo kwake.
Ndiyo …. Alituumba tofauti lakini hakuna aliyefanywa akawa na ukuu kuliko mwingine.
Siso sote tu sawa mbele zake.
Waweza kutangulia maishani; lakini kutangulia sio kufika.
Waweza kufika mbele lakini usimcheke aliye nyuma.
Baraka zake kweli ni za ajabu… Lakini Baraka sio kipimo cha nani Bora.
Kwani yeye hufanya kila kitu kiwe zuri kwa wakati wake  

Posts created 45

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Posts

Begin typing your search term above and press enter to search. Press ESC to cancel.

Back To Top